Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenge Jazz kuzindua video mbili leo

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Huwezi kuanza kuelezea historia ya muziki wa dansi nchini pale utakapolisahau jina la bendi ya JWTZ, Mwenge Jazz, inayopiga muziki wake katika mtindo wa Paselepa.

Leo, Machi 23 katika ukumbi wa Club 361 kundi hilo linazindua video za nyimbo zao mbili ‘Usiende Kombo’ na ‘Heshima yangu’ wakisindikizwa na mwanamuziki Christian Bella na JKT Kimbunga.

Akizungumza na Mwananchi mratibu wa onyesho hilo Selemani Semunyu amesema Mwenge Jazz itazindua video zao huku ikiwatambulisha wanamuziki wapya kwani ni chuo ambacho kila mara kinaingiza na kutoa kizazi kipya, huku wale waimbaji wazee wakiachwa kutokana na kuwa na mashabiki wao toka kitambo.

Semunyu anasema wanaamua kutumia mtindo wa kuchukua damu changa kuendana na soko lililopo kwa sasa katika muziki wa dansi.



Chanzo: mwananchi.co.tz