Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Mwasiti Almas amesema, wasanii wengi wa kikae ni wanafiki na ndio maana wanashindwa kushirikiana.
Akizungumza na vyombo vya habari juzikati, Mwasiti alisema endapo wasanii wa kike wangeacha unafiki wangefanya makubwa kwani mashabiki wanatamani kuona kazi zao za kushirikiana.
“Kuna wakati nilipewa jukumu la kuanzisha grupu la WhatsApp, huwezi amnini niliwaunga wasanii wengi lakini hakuna aliyejibu ule ujumbe nilioandika mimi wa kuwakaribisha.
“Yani watu wanakufata in box wanakuambia nimeona sister lakini hawataki kujibu kwenye grupu,” alisema Mwasiti.
Mwasiti alimaliza kwa kusema, yeye aliliona tatizo la wanawake kutokuwa na ushirikiano na ndio maana aliamua kukomaa na kolabo za wasanii wa kiume badala ya wa kike.