Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwasiti: Godzilla hakuwa rafiki wa kawaida

41613 Mwasitipic Mwasiti: Godzilla hakuwa rafiki wa kawaida

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanamuziki Mwasiti amesema ukaribu wake na Godzilla ulivuka mipaka kuwa wa kawaida na badala yake uligeuka kuwa undugu.

Akizungumza katika msiba wa Godzilla uliopo nyumbani kwao, Salasala jijini Dar es Salaam, Mwasiti amesema  ana msiba mzito kwa kuwa amepoteza ndugu wa karibu.

Amesema amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi  na rapa huyo kiasi cha kumfanya awajue ndugu yake na hata kujikuta wakibadilika kuwa wanafamilia moja.

“Nilikuwa na uhusiano na Zillah kwa muda lakini tulipoachana tukabadilika kuwa wana ndugu, huu ni msiba mkubwa kwangu kwa kuwa ni sawa na nimepoteza kaka,”  amesema Mwasiti.

Amesema tofauti na wapenzi wengine wanapoachana hugeuka maadui, kwao ilikuwa tofauti kwa sababu Godzilla alikuwa mwanamume mwenye haiba ya kipekee.

Mwasiti na Godzilla wamewahi kushirikiana katika nyimbo  Soldier na First Class.

VIDEO: Dada wa Godzilla asimulia rapa huyo alivyohangaika kabla ya kufikwa na umauti



Chanzo: mwananchi.co.tz