Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwanaume wa miaka 54 aoa mtoto wa miaka 4

Wedding Ewrf Mwanaume wa miaka 54 aoa mtoto wa miaka 4

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za watoto huko nchini Nigeria yameibuka na kuonyesha hasira zao, baada ya Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 54, kumuoa mtoto mwenye umri wa miaka minne, kwa madai kuwa ni njia ya kumuokoa na kifo.

Kwa mujibu wa mtandao wa SaharaRepoters, umeeleza kuwa baadhi ya vyanzo kwenye jamii hiyo vimesema kuwa mtoto huyo alidai kuwa mwanaume huyo ni mume wake ambaye alifariki dunia katika maisha yake ya awali na kwamba kwa miaka mingi amekuwa akihamahama kutoka sehemu moja hadi nyingine, ili kuzaliwa chini ya wazazi tofauti, akimtafuta mume wake huyo wa zamani, na endapo asingeolewa na mwanaume huyo asingekuwa na kazi nyingine katika jamii hiyo ya Akedei, na kwamba angekufa kwa amani.

Ili kuepusha kumpoteza binti huyo, chanzo hicho kimesema kuwa watu wa Akedei waliamua kuandaa sherehe ya harusi, kuashiria muungano wa wapendanao hao wawili wa zamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live