Mkongwe wa nyimbo za Pop nchini Uingereza, Spandau Ballet Martin Kemp (62) amedai kuwa amebakiza miaka 10 ya kuishi baada ya kuteseka na uvimbe kwenye ubongo.
Kwamujibu wa Tovuti ya The Sun imeeleza kuwa msanii huyo aligundulika na uvimbe huo miaka ya 90 ambapo ulikuwa mdogo na ulikuwa unahitaji upasuaji na matibabu ya awali ya mionzi lakini haikuweza kufua dafu.
Spandau ameeleza kuwa mateso hayo na njia ngumu ya kupona yalimsababishia kutafakari juu ya kifo chake na kudai kuwa kama angekuwa na uwezo angekimbia kifo hicho.
Licha ya msanii huyo kuwa na matumaini ya kuishi miaka hiyo bado ameonyesha wasiwasi juu ya afya yake ambapo hivi karibuni alisema. “Sijui nimebakiwa na muda gani lakini naamini ni mika 10, tangu nikiwa na umri wa miaka 34, nilipopitia hofu hiyo ya uvimbe wa ubongo, nilitumia miaka miwili ya maisha yangu kuwaza naenda kufa,”
Mwanamuziki huyo alipata umaarufu kupitia nyimbo za Pop kama True, Gold, To Cut a long story Short, Paint me Down, This is Love, Only when you Leave na nyengine nyingi.