Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamuziki wa DR Congo atekwa

15296 Pic+congo TanzaniaWeb

Mon, 3 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Polisi waitaka familia kutoa taarifa kituo cha polisi haraka ili jitihada za kumtafuta zianze mara moja

Wakati vuguvugu la kisiasa likiendelea Jamhuri ya Kidemokrasia Congo Msanii mmoja anayempinga Rais wa nchi hiyo ametekwa na watu wasiojulikaana.

Msanii huyo mchanga wa muziki wa kufokafoka na mkosoaji wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alipotea tangu Jumatano, msemaji wake aliliambia Shirika la Habari la AFP.

Msanii huyo Bob Elvis Masudi alitoweka tangu Jumatano wakati alipokuwa akienda nyumbani kwa mtayarishaji wa muziki wake kwa maandalizi ya kutoa albamu yake mpya.

Msemaji wa mwanamuziki huyo, Willy Kanyinda alisema mpaka sasa hakuna anayefahamu alipoenda mwanamuziki huyo kwa upande wa familia na hata wanatasnia ya muziki huo.

Hata hivyo Mkuu wa Polisi jijini Kinshasa, Sylvano Kasongo aliliambia AFP kuwa ameshangazwa na taarifa hizo kwa sababu hakuna yeyote katika familia yake aliyetoa taarifa polisi kuhusu kupotea kwake.

“Ikitokea jambo kubwa kama hilo ni wajibu taarifa zikatolewa kituo cha polisi ili jitihada za kumtafuta zianze mara moja’’alisema Kamanda Kasongo. Alisema ni vyema familia ikatoa taarifa polisi haraka ili kazi ya kumtafuta ianze lakini siyo kusikia tu kwenye vyombo vya habari.

Uchaguzi DRC

Uchaguzi Mkuu Nchini humo umetangazwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu ambapo Rais aliyeko madarakani Joseph Kabila akitangaza kwamba hatagombea tena.

Alisema mrithi wake atakuwa Emmanuel Ramazani Shadari na kwamba huyo ndiye atakayefaa kuongoza taifa hilo.

Shadari mwenye umri wa miaka 57 alitajwa kwamba ni mtu wa karibu sana na Rais Kabila.

Awali alikuwa Katibu wa Kudumu wa Chama Tawala cha PPRD na mpiga debe mkuu wa Rais Kabila.

Shirika la haki za kibinadamu la Human Rights Watch lilisema kuwa alitumia nguvu kukamata viongozi wa upinzani na wafuasi wao mbali na kukamatwa kwa wanaharakati.

Chanzo: mwananchi.co.tz