Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamuziki nguli wa Kongo afariki dunia

Tshala Muana Aa05 Ce80de7f4e8f 1 Mwanamuziki nguli wa Kongo afariki dunia

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nguli wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Elizabeth Tshala Muana (64) amefariki dunia jijini Kinshasa alfajiri leo. Chanzo cha kifo cha chake hakijajulikana mpaka sasa.

Taarifa za kifo chake kimethibitishwa na mume wa marehemu, Claude Mashala, kupitia chapisho lake la Facebook.

“Mapema asubuhi ya leo, Bwana mwema alichukua uamuzi wa kumchukua Mama wa Taifa Tshala Muana. Mungu mwema atukuzwe kwa nyakati zote njema alizotujalia hapa duniani. Kwaheri Mama,”ameandika Mashala.

Marehemu Tshala Muana alipata umaarufu barani Afrika kwa nyimbo kadhaa Zaidi kupitia nyimbo zake ‘Karibu Yangu’ na ‘Dezo Dezo’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live