mwanamuziki kutoka Kenya, Gidi Kocha amefungua hisia zake kwa kueleza kuwa anampenda muigizaji maarufu Tanzania Kajala huku akidai uzuri wake sio wa level ya kuwa na wanaume wa wakitanzania.
Mwanamuziki amedai kuwa anachukizwa na bifu na maneno yanayoendelea mitandaoni kuhusu mrembo huyo na ex wake, kutokana na hayo amedai kuwa inaonesha Kajala anapitia changamoto kwenye mahusiano yake anasema.
"Ujue Kajala ni mwanamke mzuri sana, hapa Kenya anapendwa sana. Nadhani ingefaa apate mwanaume kutoka Kenya sisi huku tuna pesa nyingi na hatuoni ubaya kuhudumia wake zetu.
Huyu mwanamke mimi nampenda sana hata kabla sijawa maarufu nilikuwa nafuatilia movies zake, huyu ni wakuweka ndani ya nyumba,"