Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamuziki Ally B afariki Dunia

Ally Bbb Mwanamuziki Ally B afariki Dunia

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Familia yake imesema aliugua ghafla na akafikishwa hospitalini Coast General ambapo alizidiwa akafariki.

Aliwahi kutamba na vibao kama Maria, na Bembea. Wanamuziki wakongwe ambao walianza sanaa na marehemu wametumia mitandao ya kijamii kutangaza kifo cha mwenzao.

“Kifo chako kimenipiga,” alisema Susumila Yusuf ambaye aliwahi kushirikiana naye.

Kulingana na wandani wake, mwanamuziki huyo aliaga dunia katika hospitali kuu ya Pwani alipopelekwa baada ya kuugua.

Aliwahi kujitosa kwenye siasa na kuwania kiti cha uwakilishi wa wadi ya Junda kupitia chama cha UDA, lakini hakufanikiwa. Wanamuziki wengine ambao wametuma rambirambi ni Jaguar na Masauti.

Mnamo Julai 27, 2021, mwanamuziki huyo kutoka Pwani aliitwa kutumbuiza kwenye hafla ya wasanii wa Mlima Kenya iliyoandaliwa na mmiliki wa kampuni ya Royal Media Services (RMS) SK Macharia.

Hafla hiyo ilifanyika Gatanga katika Kaunti ya Murang’a na kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga na mfanyabiashara wa Mombasa Suleiman Shahbal, walionekana kufurahia wimbo wa msanii huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live