Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke awabwaga wanaume shindano la kula

Emure Yam.jpeg Mwanamke awabwaga wanaume shindano la kula

Sat, 22 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Emure Yam 2022; ni shindano la kula lililojipatia umaarufu zaidi nchini Nigeria wikiendi hii ambapo safari hii mwanamke mmoja aligeuka gumzo baada ya kuwabwaga wanaume kwenye finali.

Shindano hilo lilikuwa na wanaume wengi zaidi waliokuwa wakionesha ustadi wao wa kula huku mwanamke huyo akichukua chache kumaliza mlima wa chakula ili pate tuzo.

Mwanamke huyo anaonekana kwenye video akifukia chakula hicho ambacho ni ugali wa magimbi na mboga huku akiwafunika vibaya wenzake katika shindano hilo lililohudhuriwa na watu wengi.

Watu waliohudhuria shindano hilo walikuwa wanamshabikia mwanamke huyo kwa kuibuka wa kwanza kwenye kinyang’anyiro hicho.

Wakiwa wamevalia mavazi ya kienyeji, washiriki waliketi kitako sakafuni kwenye mkeka kisha waliamriwa kuanza ambapo wengi wanaonekana wakimeza bila kutafuna.

Gumzo limeendelea kwa sababu hata mshindi wa pili alikuwa ni mwanamke huku wanaume wakibaki na mlima wa ugali.

Baadhi ya Watanzania kwenye mitandao ya kijamii wanatamani kuwepo kwa mashindano ya kula huku wengi wakiomba yawe ya kula ugali na kuku au chipsi zege na soda baridi!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live