Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwanamke anayeshikilia rekodi ya kucha ndefu aeleza changamoto

Mwanamke Anayeshikilia Rekodi Ya Kucha Ndefu Aeleza Changamoto Mwanamke anayeshikilia rekodi ya kucha ndefu aeleza changamoto

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Diana Armstrong ambaye anashikilia rekodi ya dunia ya ‘Guinness World Records’ kwa kuwa mwanamke mwenye kucha ndefu zaidi ameeleza kuwa anapitia changamoto nyingi kutokana na kucha hizo.

Kwa mujibu wa tovuti ya #DailyStar #Diana anasema anapata tabu sana anapoenda chooni, kuvaa nguo na imefikia mahali hata kuendesha gari hawezi tena.

Mwanamke huyu raia wa Marekani ambaye ana umri wa miaka 64, hajawahi kukata kucha zake tangu mwaka 1997 na hadi sasa zinaurefu wa futi 42.

“Kila kucha moja huchukuwa hadi masaa 10 kuisafisha tu, mara ya mwisho kuzipaka rangi ilikua wiki iliyopita na nilitumia siku nne" alisema #Diana

Aidha ameweka wazi kuwa kucha hizo zinakumbukumbu ya mtoto wake wa kike aliyefariki akiwa na miaka 16, siku moja kabla ya kufariki alikuwa akiziosha na kuzisafisha , hivyo anaona akizikata atakuwa ameondoa kumbukumbu ya mtoto wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live