Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamitindo wa Uganda aapa kukuza nywele zilizokatwa jela

Mwanamitindo Wa Uganda Aapa Kukuza Nywele Zilizokatwa Jela Mwanamitindo wa Uganda aapa kukuza nywele zilizokatwa jela

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Mbunifu mashuhuri wa mitindo wa Uganda ambaye nywele zake (dreadlocks) zilikatwa baada ya kukamatwa ameambia BBC kuwa ana mpango wa kuzikuza tena "muda wote [atakapoishi]".

Latif Madoi, ambaye ametengeneza nguo za watu mashuhuri kama vile msanii maarufu wa reggae wa Afrika Kusini Lucky Dube na Busy Signal wa Jamaica, alikaa kizuizini kwa zaidi ya wiki sita.

Hajapatikana na hatia ya uhalifu wowote lakini wakuu wa magereza hata hivyo walisisitiza kukata nywele za nywele ambazo amekuwa akikuza kwa miaka 17.

Siku ya Jumatatu aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja za Uganda sawa na dola 269 za Kimarekani.

Baada ya kutulia nyumbani, Bw Madoi aliambia BBC kwamba hatua ya kunyolewa nywele zake "ilikuwa tukio la kuvunja moyo".

Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 47 alipata umaarufu wake kupitia "matamasha ya mtindo" ambapo angetengeneza nguo 10 hadi 15 kwa saa mbili tu.

Lakini sasa, bila nywele ambazo zilikuwa sehemu muhimu ya utambulisho wake wa Rastafari, anahisi "aibu ... siwezi kutembelea maeneo. Huenda hata nitahisi aibu kurudi jukwaani".

Chanzo: Bbc