Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamitindo mbioni kuzindua kava za simu za kusaidia kupaka lipstick

Mwanamitindo Kava Mwanamitindo mbioni kuzindua kava za simu za kusaidia kupaka lipstick

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo kutoka nchini Marekani Hailey Bieber yuko mbioni kuzindua kava za simu ambazo zitaweza kuwasaidia wanawake wanaopenda kupaka #lipstick, kuhifadhi kipodozi hicho nyuma ya 'kava'.

'Kava' hilo ambalo limepewa jina la ‘Rhode’ litaweza kutumika na watumiaji wa simu za Iphone 14 na 15 ambapo litaghalimu dola $ 35 ambayo ni zaidi ya tsh 90 elfu.

#Rhode linatarajiwa kuanza kupatikana kupitia tovuti ya ‘Rhodeskin.com’ ifikapo Februari 27, huku mrembo huyo alieleza kuwa lengo la kubuni 'kava' hilo ni kupunguza uzito na wingi wa vitu kwenye pochi za mabinti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live