Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamitandao maarufu Nigeria ashtakiwa kwa kurusha pesa hewani

Mwanamitandao Maarufu Nigeria Ashtakiwa Kwa Kurusha Pesa Hewani Mwanamitandao maarufu Nigeria ashtakiwa kwa kurusha pesa hewani

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Mwanamitandao maarufu nchini Nigeria na mfanyabiashara Cubana chief priest amekuwa wa hivi punde zaidi kushtakiwa kwa kutumia vibaya pesa za noti.

Mwanamitandao huyo, ambaye jina lake halisi ni Pascal Okechukwu, alikana mashtaka matatu ya kutumia vibaya noti alipofikishwa mahakamani Jumatano.

Mamlaka zinasema alirusha pesa hewani katika hafla mbalimbali za kijamii.

Hili kimsingi ni kosa kwani noti huanguka chini ambapo zinaweza kukanyagwa.

Kitendo hicho, "maarufu", mara nyingi hufanyika katika harusi na sherehe za Nigeria.

Pesa hutupwa hewani na kuanguka chini ambapo wageni huanza kuokota.

Siku ya Jumanne, shirika mashuhuri la kupambana na uhalifu nchini Nigeria, Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha (EFCC), ilisema inaongoza harakati dhidi ya "aina zote za matumizi mabaya ya naira [fedha]".

Chanzo: Bbc