Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwana FA awaahidi makubwa wasanii

9cc381dbea131028711420075ddcd18b Mwana FA awaahidi makubwa wasanii

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA ubunge wa CCM katika Jimbo la Muheza, Hamis Mwinjuma (pichani) maarufu Mwana FA, amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge atatea haki za wananchi na wasanii katika Bunge.

Mwana FA ambaye ni msanii nyota wa Hip hop, alisema hayo mwishoni mwa wiki baada ya kuchukua fomu ya kuwania ubunge kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

Alisema wasanii wana mahitaji mengi amabyo hayajashughulikiwa, hivyo akiingia bungeni atahakikisha pamoja na kuwatetea wananchi wa Muheza, pia atasimamia wasanii wote nchini ili wapate haki zao.

“Wasanii wana mahitaji, lakini hayajatekelezwa, hivyo nikiingia bungeni nitahakikisha napambana kuwawezesha kupata haki zao, ikiwamo kukomesha kudhulumiwa haki zao,” alisema.

Mwana FA anajulikana kwa vibao kibao vikiwamo Mabinti, We endeleo tu, Bado Nipo Nipo, Ahsanteni kwa Kuja, Habari Ndio Hiyo, Unanitega, Hata Sielewi, Ingekuwa Vipi na Hawajui.

Msanii huyo, alisema atashirikiana vizuri na wananchi wa Muheza katika kutatua changamoto zao zinazowakabili.

Chanzo: habarileo.co.tz