Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwana FA aliwahi kuwa 'Black Skin'

Vicho Mwana FA aliwahi kuwa 'Black Skin'

Wed, 5 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Kabla ya East Coast Team, mwanamuziki na Mbunge wa Muheza, Mwana FA alikuwa member wa kundi la 'Black Skin', ambalo alijiunga nalo tangu akiwa shule tanga 1995.

Kundi la Black Skin lilikuwa likiundwa na wasanii watatu ambao ni Robby Ras, Generics na Mwana FA, walikuwa wakishiriki mashindano mbalimbali kama 'Tanga Hip-Hop competition' na walifanikiwa kushinda tuzo ya mshindi wa tatu.

Kipindi hicho Mwana FA alikuwa anasoma Tanga, Kundi lake la “Black Skin” lilikuwa linashindana sana na kundi lingine kwa kipindi hicho ambalo lilifahamika kama “Rough Niggas”.

Mwana FA alianza kujikita kwenye muziki akiwa na umri wa miaka 12, huku ushawishi mkubwa aliendelea kuupata kutoka kwa watoto wa shangazi yake ambao walikuwa wanafanya muziki kipindi hicho, na wao walikua na kundi la rap lilifahamika kama Quite Gangster Chronic (QGC).

Robby Ras na Generics wote wawili kwa sasa wameacha muziki.  

Chanzo: eatv.tv