Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwana FA ajiingiza kwenye biashara ya manukato

32454 MWANAFAPIC Mwana FA akiwa na Rais Mstaafu Kikwete

Wed, 19 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanamuziki Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA ametangaza kuingiza sokoni manukato yake yaitwayo FYN kuanzia wiki ijayo.

Staa huyo anayetamba na wimbo Hata Sielewi anasema ameona kuna haja ya kuanzisha biashara hiyo ili watu wanukie vizuri.

“Nimeona na sisi tunukie tu vizuri kwani kitu gani bwana! Waungwana, ndugu zangu wapendwa, body sprays (manukato) zitakuwa sokoni kuanzia wiki ijayo,”ameandika msanii huyo katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha za manukato hayo.

 

Kwa hatua hiyo Mwana Fa anaendelea kuongeza idadi ya wasanii wenye bidhaa zao sokoni kwani jana, supastaa Vanessa Mdee naye alizindua viatu kwa ajili ya wanafunzi.

Wengine ambao tayari wana bidhaa zao sokoni ni Jux, Alikiba, Wema Sepetu, Diamond, Aunty Ezekiel na Riyama.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz