Mwanaume mmoja nchini China amerekodiwa akijisaidia haja ndogo kuelelekea kwenye tenki katika Kiwanda cha Bia aina ya Tsingtao.
Video hiyo ilimuonyesha mwanaume aliyevaa kofia na gwanda la bluu akipanda hadi kwenye tanki lenye kimea katika Kiwanda hicho, mara alifungua zipu ya suruali na kujisaidia.
Tetesi zinadai kuwa mtuhumiwa wa tukio hilo si Mfanyakazi wa Kiwanda hicho bali ni mpakiaji aliyeajiriwa na Kampuni nyingine ambayo ni washirika wa Tsingtao.
Tsingtao ambayo kwa mujibu wake ni Kampuni sita kwa ukubwa katika utengenezaji Bia duniani imesema kuwa imelazimika kuufungia mzigo wote uliohusika na tukio hilo.
”Kampuni yetu imeichukulia kwa umakini mkubwa video ya tarehe 19 Oktoba iliyosambaa kutokea kwenye moja ya viwanda vyetu”
Kiwanda hicho kimeanza uchunguzi rasmi kuhusiana na tukio hilo ambalo tayari limeshaathiri shea za kampuni katika soko la hisa la Shanghai.
Ijumaa iliyopita shea zilikuwa zimeshuka kwa asilimia 1 na hadi jana asubuhi zilkuwa zimeshashuka kwa asilimia 7.5
”Tumekwisharipoti tukio hilo kwa polisi na mamlaka za usalama wa umma zimo kwenye uchunguzi”.