Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamba apata zali la mentali, amnyakua mrembo tajiri

Blessings Kaliati Mwamba apata zali la mentali, amnyakua mrembo tajiri

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Blessings Kaliati; ni jamaa wa Malawi mwenye makazi yake Capetown nchini Afrika Kusini ambaye amepata zali la mentali baada ya kumvutia kimapenzi mwanadada tajiri kutokana na unyenyekevu na wema wake.

Kaliati alihama kutoka Malawi kwenda Afrika Kusini na kufanya kazi ya bustani katika nyumba ya mrembo huyo.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Face of Malawi, wakati akifanya kazi kwenye nyumba hiyo, kila mrembo huyo alipokuwa akienda kazini, mchumba wake ambaye hakuwa na kazi, lakini ametoka katika familia ya kitajiri, alikuwa akiwaleta wasichana wengine nyumbani hapo na kufanya yao.

Mchumba huyo alifanya hivyo kwa miezi kadhaa hadi siku moja, akamfumania na kumaliza uhusiano huo kwa kumfukuza kutoka katika nyumba yake na alivunjika moyo akibaki mpweke na huzuni.

Kaliati alipoona kwamba boss lady huyo alikuwa amevunjika moyo na hakuwa ametoka nyumbani kwa siku nyingi ndipo akaanza kumfariji.

Kaliati alianza kumuandalia chakula, kumpa msaada wa kihisia, kumsimulia hadithi kuhusu Malawi na jinsi alivyohamia Afrika Kusini licha ya kuwa na elimu na kadhalika.

Wawili hao walianza kuelewana na kadiri siku zilivyosonga Kaliati alijikuta hafanyi kazi tena kama garden boy, bali anachofanya ni kuonesha mapenzi kwa madam.

Alijikuta akiwa mtu wa kumuandalia chakula, anaosha vyombo, anampigia muziki, anasimulia hadithi na kumjali sana.

Kwa upande wake, Boss Lady akawa anamtunza vizuri kipesa, kihisia na kimwili; watoto wa mjini wanasema amepata zali la methali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live