Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwamba ampachika mimba mama yake, mkewe aruhusu

Nancy Hauk 1663926836 Mwamba ampachika mimba mama yake, mkewe aruhusu

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika miaka ya zamani na leo, watoto huchukuliwa kama zawadi kwa familia, Mama mjamzito hutunzwa kama yai. Mtoto hua mwanga wa furaha kwa wanandoa.

Nchini Marekani, mwanamke mwenye umri wa miaka 56, Nancy Hauck kutoka eneo la Utah anakila sababu ya kutabasamu wiki chache zijazo atakapojifungua mtoto wa mwanae wa kumzaa, hii ni baada ya kugundua mkazamwana hana uwezo wa kushika mimba.

Jeff (32) na mke wake Cambria (30) ambao ni wazazi wa watoto wanne walikuwa wamehangaika kupata mimba kwa miaka sita kabla ya kupata mapacha, Vera na Ayva wa miezi 11 kisha Diseal na Luka kwa njia ya kupandikiza (Intra Vitro Fertilisation -IVF).

Hata hivyo, mipango yao ya kuwa familia kubwa iligonga mwamba mwaka jana kufuatia upasuaji wa kuzaliwa kwa mapacha hao.

Baada mamake Jeff, Nancy ambaye ni mmoja wa viongozi wakubwa huko St. George kujua hali yao, aliingilia kati na kujitolea kuwasaidia baada ya kujua kwamba anaweza kujifungua licha yake kuwa mkongwe.

"Sikuwahi kufikiria hili litafanyika, lakini baada ya mkewe Jeff kujifungua kwa dhiki na kuniomba nimbebe mtoto wao. Niliwaambia niko tayari lakini ningali mzee. Lakini baada ya kushauriana na madaktari walisema mimi ni mzima na nina afya njema.

"Jeff na mume wangu (baba wa Jeff) wamekuwa wakishangaa imewezekanaje, na sasa nina furaha kumbebea mwanangu kichanga chake cha kike. Ni sawa na kubeba mtoto wangu," Nancy aliiambia kituo kimoja cha habari huko Marekani.

Sasa baba wa familia hiyo yupo tayari kumpokea mtoto wake wa tano.



Cambria, ambaye ni mmiliki wa dance studio, amesema: " Ni heshima kubwa kwa mama mkwe wake kwa kutufanyia jambo kubwa kama lile. Amejitolea kwa ajili yetu, na familia yetu. Ninajisikia mwenye faraja sana.

"Imekuwa kama miujiza na baraka kumuona Nancy akibeba ujauzito wa mtoto wetu wa kike.

Jeff amesema: "Najisikia mwenye furaha kuona napiga picha ya selfie na mama yangu kipenzi ambaye amejitolea kwa ajili ya familia yangu. Nimejaribu kwa miaka minne kutafuta kizazi, nafahamu kazi ilivyokuwa ngumu kwetu, lakini mama yangu kwa upendo wake ameamua kutuheshimisha," amesema Jeff.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live