Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwamba afunga ndoa na wanawake watatu siku moja

Mwamba Huyu Mwamba afunga ndoa na wanawake watatu siku moja

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Athumani Yengayenga (35), mkazi wa Shanwe Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, amewashangaza watu wengi kwa kuamua kufunga ndoa na wanawake watatu kwa siku moja huku akidai lengo lake lilikua ni kufunga ndoa na wanawake wanne kwa siku hiyo.

Hali hiyo imeibua maswali na mshangao kwa wakazi wa Mpanda na jamii kwa ujumla ambapo baadhi ya watu wamesema tukio hilo nilakwanza kutokea kwa Katavi na Tanzania kwa ujumla.

Akizungumzia ndoa yake Bwana harusi huyo amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na maumivu aliyoyapata mwanzo ya kuachwa na mke mmoja Aliekua amemuoa.

Amesema baada ya kuachwa na mke wake huyo aliona kuna umuhimu wa kuoa wanawake wanne ili ikitokea ameachwa na mmoja atabakia na wake watatu ndipo alipoanza kazi ya kuwatafuta wanawake hao kwa nyakati tofauti.

Amesema alitumia saa nne kukaa kikao na wanawake hao ili kuwashawishi wakubaliane na wazo lake la kufunga ndoa na wote watatu kwa siku moja hivyo kufikia Julai 8, 2023 alifanikiwa kufunga ndoa hiyo katika msikiti mkubwa wa ijumaa uliopo mjini Mpanda.

Wanawake hao wamesema wamefurahi kuolewa na wanaona jambo la kawaida japo mwanzo ilikua ni jambo gumu kulipokea hasa kwa mke mkubwa alipofikishiwa suala hilo na mume wake.

Mashaka Kakulukulu ni Shekh wa Mkoa wa Katavi amekili kufungisha ndoa hiyo huku akidai imefuata taratibu zote za dini na ametofautisha muda katika kufungisha ndoa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live