Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwamba adanganya amezimia ili kukwepa kulipa bili ya mgahawa

Mwamba Ziraii Adanganya amezimia ili kukwepa kulipa bili ya mgahawa

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mmoja raia wa Lithuania amekamatwa baada ya kudanganya kupata mshtuko wa moyo katika migahawa isiyopungua 20 aliyoingia Nchini Uhispania ili kukwepa kulipa bili ya chakula.

Mtu huyo ambaye jina lake halijawekwa wazi mwenye umri wa miaka 50 aliripotiwa kulaghai takriban migahawa 20, nyingi zikiwa katika eneo la Costa Blanca nchini Uhispania, kwa kughushi mshtuko wa moyo.

Baada ya kuagiza chakula na vinywaji, alicheza mchezo huo wa kuigiza kwa kujishika kifua na kujifanya amezimia sakafuni. Ulaghai huo uliendelea kufanya kazi hadi pale mmiliki mmoja wa mgahawa alipoona kitendo cha mtu huyo na kuchapisha picha zake kwenye mikahawa mingine ya eneo hilo kama onyo.

"Ilikuwa kama tamthilia, alijifanya kuzirai na kujilaza chini," meneja wa mgahawa mmoja alisema.

Mmiliki mwingine wa mgahawa alisema kwamba mtu huyo aliagiza glasi kadhaa za whisky na saladi kabla ya kughushi kupata mshtuko wa moyo.

Alifungwa jela kwa siku 42 baada ya kukataa kulipa faini mbili kuhusiana na mfululizo wake wa matukio yake ya kula na kudanganya kuzimia.

Wakili mmoja alisema kwamba kwa kuwa kila tukio kilichukuliwa kuwa kiasi kidogo cha pesa, zinachukuliwa kama makosa madogo tu na haziwezi kusababisha hukumu ndefu zaidi.

Hata hivyo wamiliki wengine migahawa wanatafuta kuwasilisha malalamiko ya pamoja ambayo yanaweza kumweka gerezani kwa miaka miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live