Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwalimu atupwa jela kwa kumtumia picha za utupu Mwanafunzi

Mwalimu Mwanafunzi Mwalimu atupwa jela kwa kumtumia picha za utupu Mwanafunzi

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mwalimu wa shule ya Edward Franklin Green Junior, iliyopo Texas, Joshua Hockless mwenye umri wa miaka 25 amehukumiwa mwaka mmoja gerezani kwa kujaribu kumshawishi kimapenzi na kumrushia video za utupu mwanafunzi.

Inaelezwa kuwa mwalimu huyo alimfata mwanafunzi huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuanza kumshawishi kuwa naye kimapenzi na kisha akamtumia video zake za utupu huku akimuomba pia mtoto huyo atume zake.

Mwalimu huyo hakuishia kwenye video inadaiwa pia alijaribu kumshawishi mtoto huyo kumnunulia vitu avipendavyo, huku akijaribu kumuuliza kama nyumbani kwao kuna ‘kamera’ ili aweze kwenda kukutana na mwanafunzi huyo.

Hata hivyo mwanafunzi huyo alimshirikisha mama yake yanayoendelea na ndipo mama huyo aliendelea ‘kuchati’na mwalimu kwa lengo la kupata ushahidi wa kutosha, ambao ndiyo aliutumia alipoenda kumshitaki mwalimu huyo kwa kumshawishi kimapenzi binti yake.

Tofauti na malalamiko ya mama huyo walimu wengine pia shuleni hapo walikuwa wakimlalamikia mwalimu huyo kwa sababu wanafunzi wao wa kike walikuwa wakikwepa kuingia kwenya madarasa yao na kilazimisha kuingia darasa la mwalimu huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live