Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mwalimu asimamishwa kazi kisa Ubaguzi wa Rangi

Mwalimu Afukuzwa Mwalimu asimamishwa kazi kisa Ubaguzi wa Rangi

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu wa kidosi (mhindi) aliyefahamika kwa jina la Tayabah Jadwat, anayefundisha shule ya Curro Academy Protea Glen iliyoko huko Soweto nchini Afrika Kusini, amesimamishwa kazi kufuatia tuhuma za ubaguzi wa rangi.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, alidaiwa kuwaita wanafunzi watatu nyani baada ya wanafunzi hao kuwa wasumbufu darasani jambo ambalo lilifanywa siri na walimu wenzake mpaka lilipokuja kubumburuka hivi karibuni.

Katika taarifa yake Curro Holdings mmiliki wa shule hiyo, alisema alifahamu kuhusu tukio hilo Ijumaa iliyopita na kuanzisha uchunguzi ambapo inaaminika tukio hilo lilitokea katika muhula wa kwanza wa mwaka jana.

"Kutokana na taarifa za tuhuma hizo, Curro amemsimamisha kazi mwalimu mara moja na kuanzisha uchunguzi wa kinidhamu kwa mujibu wa sera na taratibu za kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live