Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakyembe azungumzia kanuni mpya za Basata

11435 Waziri+pic TanzaniaWeb

Sun, 15 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, amesema kanuni wanazolalamikia wasanii za tozo mbalimbali hazikuja kwa bahati mbaya.

Akizungumza leo Julai 14 na wanahabari pamoja na wasanii, Dk Mwakyembe amesema vikao mbalimbali vilikaa na kupitisha kanuni hizo.

Hivi karibuni Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) lilitangaza kanuni mpya zinazotaka waandaaji wa maonyesho ya wanamuziki, kulipa kuanzia Sh50,000 hadi Sh5 milioni. Sheria hizo zilianza kutekelezwa Julai Mosi.

Aliwalaumu wasanii wengi wenye majina makubwa kutohudhuria vikao.

"Wasanii hamuhudhurii vikao, mnasubiri kuja kulalamika sheria na kanuni zikishapitishwa, kwani wengi mkishapata majina mnapandisha mabega juu na kujiona nyie ndio nyie hata mkiitwa katika mambo yenye faida kwenu hamji,”amesema.

 Mwakyembe alimtaja Wakazi (jina halisi Wabiri Wassira)  na kueleza kuwa hajawahi kumuona katika vikao vya wasanii.

Mmoja wa wasanii hao alimtaja kuwa ni Wabiri Wassira'Wakazi', ambapo alidai katika vikao tisa ambavyo amewahi kuitisha vya wasanii hajawahi kumuona na kumuuliza labda kama anishi Ulaya.

Pia, alishangaa kwa nini tangu kanuni hizo zipitishwe,wanaopiga kelele ni wasanii na siyo kampuni.

Soma Zaidi:

Kanuni za malipo Basata zapingwa kila kona

 

Chanzo: mwananchi.co.tz