Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo amkumbuka Ruge

Mwakinyo Ruge Mwakinyo amkumbuka Ruge

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia namba moja nchini Tanzania, Hassan Mwakinyo amemkumbuka aliyekuwa mdau nguli wa sanaa ya muziki nchini, marehemu Ruge Murahaba.

Hii inakuja baada ya Mwakinyo kufungiwa kujihusisha na mchezo wa ngumi kwa ndani na nje ya Tanzania na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) baada ya kugomea pambano lake la hivi karibuni.

"Wapo waliowahi kusema marehemu Ruge alikua mkandamizaji, mnyonyaji na aliwabana sana wasanii wa muziki na sisi wengi ambao tulichelewa kumfahamu marehemu tuliamini ni kweli.

"Lakini cha ajabu amekufa na muziki umekufa hata kwa waliohisi kubanwa na uwepo wake ispokua umebaki kwa watu wa chache, hii ni nini.

"Hii ni ile tafsiri isemayo ya kua usitarajie usicho nacho kwa ukubwa wako’ vitu na mambo huwenda kwa nguvu ya Qadar, kesho imebeba tumaini kubwa mioyoni mwa wengi ni kweli lakini haituhakikishii vya kutosha kuyafanya tulio yashindwa leo.

"Mogadishu Family, watu kama mjomba Mrisho Mpoto watakua wamenielewa deep, sana Kennell," amesema Mwakinyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live