Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwaka mmoja tangu kifo cha Ivan; ‘Najua unatabasamu katika utukufu wa Mungu’ – Zari

8357 Zari Ivan Don Bongo5 Pix 1 TZW

Fri, 25 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Ni mwaka mmoja sasa umepita tangu aliyekuwa mume wa Zari The Boss, Ivan Ssemwanga ‘Ivan Don’ afariki.



Zari ameeleza jinsi anavyomkumbuka Ivan ambaye walijaliwa kupata watoto watatu pamoja. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika;

Mwaka mmoja umepita tangu siku hiyo ya kusikitisha ulipoitwa. Mungu alikuchukua nyumbani kwake, ilikuwa mapenzi yake lakini katika nyoyo zetu bado unaishi.

Najua kwa hakika kwamba hatuwezi kupoteza watu tunaowapenda wanapokufa. Wanaendelea kushiriki katika kila jambo, mawazo na uamuzi tunayochukua.

Upendo wao unaacha kitu katika kumbukumbu zetu.

Mimi na vijana wangu tunapata faraja kwa kujua kwamba maisha yetu yamejitosheleza kwa upendo wako. Wale tunaowapenda hawaondoki wanatembea nasi kila siku. Hawaonekani, hasikikii lakini kila siku wapo karibu nasi, bado tunawapenda na tunawakumbuka.

Najua unatabasamu kutoka katika utukufu wa Mungu. Endelea kupumzika kwa amani Don

Chanzo: bongo5.com