Inasemekana kuwa mvuvi huyo Kiindonesia anadai kushiriki urafiki na mamba huyo wa maji ya chumvi mwenye urefu wa mita nne kwa zaidi ya miaka 20 na kuwaita wanyama hao kuwa kama sehemu ya jamii ya eneo hilo.
Bw.Ambo mwenye umri wa miaka 59, mvuvi kutoka Jiji la Bontang, huko Kalimantan Mashariki mwa Indonesia, amekuwa mtu mashuhuri katika nchi yake kwa sababu ya urafiki wake usio wa kawaida na mamba huyo mkubwa aliye pewa jina la Rizka.
Mamba huyo amekuwa sehemu ya maisha ya Ambo kwa miaka 26 iliyopita, tangu alipomtazama baada ya kukutana nae kwa mara ya kwanza kwenye maji huko Pupuk Kaltim na wakati huo alikuwa na ukubwa wa mita moja tu na hakumuogopa sana alipokuwa akiogelea karibu na mashua yake, lakini alipoona kwamba alikuwa amemfuata nyumbani, Ambo alichukua chakula na kukitupa majini na huo ukawa mwanzo wa urafiki mzuri uliodumu kwa miaka 26.
“Nilikutana na Rizka mara ya kwanza nilipokuwa kwenye mashua nikipita kwenye maji ya eneo la Pupuk Kaltim miaka 23 iliyopita,” Ambo alimwambia Kompas mwaka wa 2020.
“Wakati huo alikuwa na urefu wa mita moja, kwa hivyo nilimpuuza kama nilivyofanya lakini niliona kwamba [Rizka] alifuata chombo changu hadi nyumbani.Nilimwona hata karibu na boti, ambayo pia niliipa jina la Rizka.Nikamuita ili kumpa chakula, na akaja karibu. tangu wakati huo amekuwa akifanya hivyo.”
“Ikiwa sitamwona kwa siku mbili au tatu, ninaenda kumtafuta,” Ambo aliongeza. “Ninamchukulia kama mtoto wangu mwenyewe.”