Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muziki wa hip hop umekuwa biashara, tunawekeza ili utulipe – Jay Moe

8577 Instagram Post By Jaymoe Mchopanga BTGaTWFjurG 696x696 TZW

Mon, 4 Jun 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Jay Moe amedai kwa sasa kuna vitu vingi ambayo vimebadilika kutoka wa wasanii wa muziki wa hip hop kutoka na muziki kubadilika na kuwa biashara tofauti na zamani.



Rapa huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Bata’, amedai kwa sasa kila pesa ambayo inawekezwa kwenye muziki inatakiwa kurudi.

“Sasa hivi tunawekeza sana kwenye muziki tofauti na miaka ya zamani tunatoa wimbo tu hakuna uwekezaji wowote ambao tulikuwa tunaweka,” Jay Moe alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha Efm. “Lakini sasa hivi au miaka ya sasa hivi muziki umekuwa biashara, kwahiyo lazima pia unavyowekeza uhakikishe uwe na target nzuri ya kuweza kujua pesa yangu itarudi vipi,”

Moe ni mmoja kati ya wasanii wakongwe ambao wameweza kurudi kwenye game baada ya kukaa kando kwa muda mrefu.

Loading...
Chanzo: bongo5.com