Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muziki ulivyobadili majina ya watu

WhatsApp Image 2021 05 20 At 13.39.47.jpeg Muziki ulivyobadili majina ya watu

Thu, 20 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Kuna baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva walilazimika kubadilisha majina yao ya awali waliyokuwa wakiyatumia kutokana na sababu mbalimbali huku wengine zikitajwa kuwa ni za kibiashara zaidi. 

Mwana FA – wakati ameanza safari yake ya muziki alikuwa akitumia jina lake halisi 'Hamis', lilidumu kwa muda mpaka alipokutana na mtayarishaji wa muziki Dj Boni Luv ambaye anatajwa kuwa ndiye mtayarishaji wa kwanza kuzipika kazi za Mwana FA.

Jina la Mwana FA lilitokana na wimbo uliokuwepo kwenye album yake ya kwanza uitwao Mwana Falsafa na DJ Boni Luv ndiye aliyependekeza aitwe hivyo msanii huyu wa Hip Hop Bongo.

Mr Blue – Kama ulikuwa hufahamu zamani star huyu wa Bongo Fleva alikuwa akitumia jina la ‘Lil Sama’ na lilidumu mpaka pale alipokuja na wimbo wake wa kwanza kwenye game 'Blue Blue' ndipo likazaliwa jina hili la sasa la Mr. Blue.

Barakah The Prince – Kipindi yupo Mwanza kuna siku alimpigia simu legend Prince Dully Sykes akihitaji ampatie jina ambalo angelitumia kwenye sanaa.

Dully (Mr Misifa) aliahidi kumpatia jina moja kati ya majina yake ndipo akampatia 'Prince' ambalo analitumia mpaka sasa, awali alikuwa akitumia jina lake halisi ‘Barakah’.

Young Killer – Chimbuko la jina lake ni baada ya kukutana na rafiki zake studio, kila mmoja alionesha uwezo wake wa kuchana (rap) ndipo akatokea rafiki yake mmoja hapo studio ‘Mo Chela’ (marehemu kwa sasa) akampatia jina la Young Killer kutokana na uwezo mkubwa ambao aliuonesha wa kuchana kiasi cha kuwafunika wasanii wenzake wengi waliokuwa pale.

Katika harakati zake za kujitafuta kwenye muziki alikuwa akitumia jina la ‘Lil K’ (Lil Kassim).

Professor Jay – Wakati ana anza ku-rap miaka ya 90’s alikuwa akiitwa Nigga J lakini kadri muda ulivyosogea alibadilisha jina lake na kuliacha la awali, uandishi wake na uwezo wake mkubwa kwenye muziki ulirahisisha kueleweka kwa kazi ya muziki mtaani.

Sugu – Majina haya (Mr. II na 2-Proud ) aliyapata kutokana na umahiri wake aliounesha kwenye muziki wa Hip Hop Bongo.

Chanzo: eatv.tv