Ramadhan Juma (25) elimu yake ni darasa la saba ni miongoni mwa vijana wanaoishikilia medani ya Upambanaji yeye baada ya kuona maisha ya kuajiriwa yana changamoto aliamua kuachana nayo na kuanza biashara yake ndogo ya kutembeza mishikaki kwenye toroli.
Ramadhani anasema baada ya suala la kusoma kutoeleweka aliondoka nyumbani na kuanza kuuza maji kwenye mifuko, aliuza kahawa, karanga, sigara na sasa anauza mishikaki inayompatia faida ya zaidi ya 30,000/= kwa siku.
“Nilianza na nusu kilo ya nyama nilikuwa nazungusha sometime nabakiza kama miezi minne sasa nimepanda nachukua kilo sita na nilichokigundua vijana wengi wanaosoma wanaishi kwa ndoto wanasema nataka niwe kama fulani, ukiishi kwa ndoto utasugua sana” Ramadhan