Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muumin sasa `ala’ fenesi

954950924439497be7507306edd1ba95 Muumin sasa `ala’ fenesi

Thu, 4 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MUIMBAJI mahiri wa muziki wa dansi nchini, Prince Muumin Mwinjuma ametambulisha kibao chake kipya cha Fenesi akiwa mbioni kuzindua albamu yake mpya.

Mwinjuma ambaye kwa sasa yuko na kundi la Special Band ambalo bado hajalizindua rasmi alisema mbele ya waandishi wa habari jana kuwa kibao cha Fenesi tayari ameshatengeneza video yake na wakati wowote itaanza kuonekana katika Yutube.

Alisema kuwa kibao hicho analizungumzia tunda fenesi, ambalo linahitaji ufundi kulila, lakini yeye halipendi kwa kuwa lina utomvu na lazima kwanza ulipake mafuta kama unataka kulila vizuri.

Alisema tunda hilo lazima ulipake mafuta ndio utaweza kulila vizuri, ingawa kwa wengine ni kero kubwa.

Vibao vingine ambavyo vimeshatolewa na Special Band ni pamoja na Yatima Mzee na Mwananngu huku kubao cha Kwa Mpalange Sihami anatarajia kukitoa mwezi ujao pamoja na Jibwa la Kizungu wakati Vumbi la Kongo, ambacho kitaimbwa na Salma kitatoka baadae.

Wasanii Muhogo Mchugu pamoja na Mzee Korongo wamepamba video hiyo ya kibao cha Fenesi wakionekana wakilichambua, wakilipaka mafuta kabla ya kulila tunda hilo.

Mbali na Salma baadhi ya wanamuziki wengine wanaounda kundi hilo ni pamoja na Rashid Sumuni, Michael Liloko, Mussa Muumin, Muumin Junior, na wengineo, ambao wanaounda kundi hilo.

Muumin aliyewahi kutamba na bendi za Mchinga Sound, The African Revolution au Tam Tam, Double M Sound na zingine alisema kuwa amekuja kivingine na ni matarajio yake makubwa kuwa atapokewa vizuri na mashabiki na madau wa muziki nchini.

Chanzo: www.habarileo.co.tz