Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muumin aibuka na Pole Mama Samia

Ba803e6923ec425bf4a9ce60c2445a44.jpeg Muumin aibuka na Pole Mama Samia

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MUIMBAJI mahiri wa muziki wa dansi nchini, Mwinjuma Muumin ameibuka na kibao cha maombelezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, Dk John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.

Muumin aliyewahi kutamba na makundi ya muziki ya Double M Sound, African Revolution, Victoria Sound, The African Stars àu Twanga Pepeta na sasa The Current Band, amerekodi kibao cha Pole Mama Samia.

Akizungumzia kibao hicho ambacho jana alikamilisha kushuti video, Muumin alisema amempa pole Mama Samia kutokana na msiba mzito, kwani yeye sasa ndiye Rais, hivyo msiba huo huko chini yake.

“Nimekuwa tofauti kidogo na wasanii wengine, kwani mimi nimempa pole Mama Samia kutokana na msiba mzito wa aliyekuwa mtangulizi wake, Dk John Magufuli, hivyo kwakuwa yeye ni kiongozi wa nchi sasa, msiba wote uko chini yake.”

Alisema Mama Samia pamoja na yote amemtia moyo na kusema kuwa watu wana matumaini naye kuendeleza mazuri yaliyoachwa na Dk Magufuli.

Muumin akimzungumzia Dk Magufuli alisema kuwa alikuwa mtu asiyeyumba katika misimamo yake na hasa ile ya kuwatetea wanyonge, ambao awali walikata tamaa, lakini baada ya kuingia madarakani wamekuwa na matumaini makubwa.

Muumin alisema kuwa Magufuli hakuwa mtu wa kuyumbishwa hata mara moja, kwani alikuwa na msimamo thabiti kwa kile alichokiamini.

Alisema kuwa Magufuli amefanya mengi na Muumin alikuwa shabiki yake mkubwa kutokana na yale aliyoyafanya, hasa kuwatetea wanyonge wakiwemo wasanii na watanzania wote kwa ujumla.

“Mimi binafsi nilikuwa shabiki mkubwa wa Magufuli na hakuna ubishi kuwa alikuwa mtetezi wa wanyonge pamoja na mali za nchi mfano alijenga ukuta Mererani ili kuhakikisha madini ya Tanzanite hayapotei, “alisema Muumin.

Akizungumzia kibao hicho, msanii huyo alisema kuwa kina mapigo kama kibao cha Kilio cha Yatima alichitunga akiwa Double M akimlilia baba yake mzazi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz