Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Museveni aanzisha sheria ya kuoga na kutakata kabla ya kuingia Kampala

Museveni Aonya Dhidi Ya 'upuuzi' Wa Wapenzi Wa Jinsia Moja Nchini Uganda Museveni aanzisha sheria ya kuoga na kutakata kabla ya kuingia Kampala

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya jiji kuu la Uganda, Kampala imependekeza sheria mpya itakayotaka watu kuoga na kujitakatisha kabla ya kupewa kibali cha kuingia katika jiji hilo kwa shughuli zao.

Kulingana na jarida la Daily Express la nchini humo, mtu mmoja ambaye anafanya kazi katika uongozi wa mamlaka hiyo alifichua pendekezo hilo linalolenga kusafisha hewa iliyojaa jijini baada ya ripoti ya hivi majuzi kuangazia kuwa harufu ya mwili ndio chanzo kikuu cha uchafuzi wa hewa katika Jiji la Kampala.

Chanzo hicho kilikiri kwa jarida hilo kwamba wanasayansi wa mazingira wa mamlaka hiyo "walifanya uchunguzi wa kina na pia waliwahoji watu ndani ya Jiji na kufikia hitimisho kwamba njia moja ya kuboresha hali ya hewa huko Kampala ni kwa kuwalazimisha watu kuoga.

Kwa maana hiyo, chanzo hicho kinasema, sehemu kadhaa za kuoga zitajengwa sehemu za barabara kuu zinazoingia mjini ambazo zitakuwa za lazima kwa wote wanaoingia mjini kuoga.

"Tumejenga vituo 24 vya kuoga kwenye barabara kuu zote za jiji. Itakuwa ni lazima kwa watu kuoga kabla ya kuingia Kampala au watazuiwa kuingia Jijini,” alisema.

"Ikiwa mtu anaoga kwenye sehemu yoyote ya kuoga," alisema, "anapokea kibali cha siku moja cha kuingia Jiji, na atalazimika kufanya vivyo hivyo siku nyingine."

Sera hiyo mpya ikipitishwa itaifanya Kampala kuwa Jiji la kwanza duniani kote kutekeleza sera ambayo inawataka watu kuoga kabla ya kuufikia.

Lakini je, hili linawezekana kwa vigezo vipi, na kama wewe unataka kwenda jijini Kampala, ungependa kupitia mchakato wa kuoga?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live