Muongozaji wa video ya Tetema, Kenny ameibuka mshindi katika vipengele viwili kwenye tuzo za All Africa Music (Afrima).
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ulifanyika jana Lagos Nchini Nigeria huku Tanzania iliwakilishwa na wasanii 11 katika vipengele mbalimbali.
Dalili za Kenny kushinda zilianza mapema baada ya wimbo huo wa Tetema kushindanishwa katika vipengele vingi.
Pamoja na wasanii wengine kutoka kapa, Kenny ameweza kuitoa Tanzania kimasomaso kwa kuibuka muongozaji bora wa video na pia kuwa videa bora ya Afrika.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram,Kenny amendika"miaka miwili iliyopita nilipoangalia tuzo za Afrima nilijiwekea ahadi kwamba siku moja nitashinda tuzo hizo.
"Asante kwa timu yangu ya Zoom Production na kwa msanii Diamond ambaye aliniamini na kufanya naye kazi,".
Katika Tuzo hizo Wasanii wengine kutoka Tanzania waliokuwa wanawania ni Maua Sama aliyeingia katika tuzo hizo kwa wimbo wake wa Ikote, Nandy (Aibu); Rosa Ree (Dip in Wine It); Vanessa Mdee (Moyo) na Queen Darleen (Mbali).
Wengine ni Diamond (Inama); Harmonize (Never give Up); Rayvany (Tetema); Mbosso (Hodari), Omy na Dimpoz (Ni wewe), kundi la Navy Kenzo katika kipengele cha Best Reggae Ragga au Dancehall kupitia wimbo wa Roll It, kipengele ambacho pia yupo Rosa Ree.
S2Kizzy, ambaye ni mtayarishaji wa muziki wa Tanzania alikuwa anawania kipengele cha mtayarishaji bora kupitia wimbo wa Tetema huku mwongozaji wa wimbo huo, Kenny naye akiwania kipengele cha mwongozaji bora wa mwaka ambacho ameibuka mshindi, ambapo pia Kipengele cha maDJ bora kilikuwa kinawania na Romy Jones