Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muongozaji wa Filamu na mkewe wauawa Iran

AP23288354506300 Muongozaji wa Filamu na mkewe wauawa Iran

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muongozaji maarufu wa filamu nchini Iran pamoja na mke wake wameuawa wakiwa nyumbani kwao nje kidogo ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Tehran.

Taarifa kutokea kwenye vyombo vya habari vya nchini Iran zinasema kuwa Dariush Mehrjui (83) na mkewe Vahideh Mohammadifar (54) aliyekuwa Mwandishi wa vitabu na mbunifu wa mavazi walikutwa wakiwa na majeraha ya visu.

Katika wiki za hivi karibuni mke wa Mehrjui alilalamika kupata vitisho vya kuchomwa visu katika mitandao ya kijamii. Binti yao Mona Mehrjui aliikuta miili yao alipoenda kuwatembelea jana usiku.

Mauaji hayo yanaweza kuleta tuhuma juu ya kuhusika kwa Mamlaka kwani hivi karibuni kumekuwa na ukandamizwaji mkubwa dhidi ya wanaoupinga utawala wa Tehran.

Kwa miaka mingi Mkurugenzi huyo alikuwa mkosoaji wa Serikali na mwaka jana alipinga kwa hasira uamuzi wa serikali wa kupiga marufuku filamu yake mpya.

Mehrjui aliyesomea masuala ya Filamu katika Chuo Kikuu cha California nchini Marekani amepokea tuzo nyingi za Kimataifa kutokana na kazi zake.

Mamlaka nchini humo zinafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na hadi sasa hakuna taarifa zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live