Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Muonekano wa kituo cha treni wazua gumzo mitandaoni

Kituo Cha Treni Muonekano wa kituo cha treni wazua gumzo mitandaoni

Sat, 4 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini China wamestaajabishwa na muundo wa kituo kipya cha treni, kituo hicho kufananishwa na taulo za kike (pedi).

Muundo huo uliyopendekezwa na kituo cha Nanjing Kaskazini ulitolewa wiki chache zilizopita ambapo uliripotiwa kugharimu dola 2.7 bilioni sawa na Sh 7 trilioni.

Aidha wabunifu hao waliweka wazi kuwa wazo la kubuni muundo huo lilikuja kutokana na maua yaitwayo ‘Plum’ ambayo ni maarufu sana katika jiji hilo la #Nanjing.

Hali ilikuwa tofauti kwa wananchi ambapo walienda mitandaoni na kufananisha muundo wa kituo hicho kama taulo za kike.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live