Kamati ya Tuzo za Muziki Tanzania 2024 (TMA) kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), wametangaza tarehe rasmi ya utoaji wa Tuzo hizo kuwa ni October 19 2024 kuanza saa nane mchana.
Tukio hilo la kipekee la Kiburudani linalotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki kuanzia saa nane mchana, linarushwa live Azam TV na AyoTV kupitia channel ya YouTUBE ya millardayo huku pia MTV na BET wakionesha matukio mbalimbali ya siku hiyo kubwa katika kiwanda cha burudani Tanzania.
Katika kikao cha leo na Wanahabari, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma pamoja na mambo mengine, amezitambulisha Tuzo zitakazotolewa siku hiyo zikiwa zimenakshiwa kwa muonekano wa Mlima Kilimanjaro.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya TMA 2024, Seven Mosha ameitaja orodha ya Wasanii watakaotumbuiza siku hiyo kuwa ni pamoja na Alikiba, Harmonize, Marioo, Young Lunya, Nandy, Zuchu, Yammi, Abigail, Salha, Christian Bella, Dula Makabila na Mzee Yusuph.