Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muna: Mungu amenitoa kwenye Umauti

MUNA Muna Love

Sat, 19 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ROSE Alphonce Nungu almaarufu Muna Love; ni mwigizaji wa Bongo Movies ambaye hajaonekana lokesheni kitambo ambaye anasema kuwa, kila siku anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu amemuinua na kumtoa kwenye umauti kisha kumrejesha uzimani.

Muna anasema kuwa, jambo hilo hakulitegemea kabisa katika maisha yake kama atasimama tena.

Hii ni baada ya kufanyiwa upasuaji (sajari) sehemu mbalimbali za mwili wake kwa ajili ya kurekebisha maumbile yake.

Muna anasema kuwa, alipita katika mapito magumu mno kiasi cha kukata tamaa, lakini Mungu amemsaidia na ameinuka na hivi karibuni atarejea tena.

“Mungu amenitoa kwenye umauti, nitarejea tena nikiwa na hofu ya Mungu. Niliyopitia ni funzo kubwa sana katika maisha yangu na nikitulia nitaelezea yote bila woga na hapo mtu ataamua kujifunza mwenyewe,” anasema Muna ambaye hivi sasa anaonekana kupona kabisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live