Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mume wa Zari adaiwa kukosa raha, kisa hiki hapa!

Zari Shakib Mume wa Zari adaiwa kukosa raha, kisa hiki hapa

Thu, 1 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi Jumanne jioni, mwanasosholaiti na mfanyabiashara Zari Hassan alichapisha picha zake kadhaa akijivinjari na mumewe Shakib Cham Lutaaya kwenye kilabu.

Zari alinukuu picha hizo akisema ni nyakati kama hizo ambapo huwa anajiachia na mpenzi huyo wa maisha yake.

"Wakati pekee utanishika nikiteleza... na mume wangu," aliandika chini ya picha hizo ambazo aliunganisha kuwa video.

Mamia ya wanamitandao walikusanyika chini ya chapisho hilo, baadhi wakitoa maoni mazuri huku wengine wakisema vibaya.

Baadhi ya wanamitandao walilalamika kuhusu tofauti kubwa kati ya umri wa Shakib na mama huyo wa watoto watano.

"Je, ni mimi tu ninayefikiria kuwa jamaa huyu ni mdogo sana?" beckleon.e alijibu chini ya chapisho hilo la Instagram.

Baadhi ya mashabiki waligundua sura ya huzuni ya Shakib na kudai alionekana kutoridhika na mwanasholaiti huyo wa Uganda.

"(Shakib) Anaonekana kukosa raha katika nyingi ya picha hizo," c_life_live alisema.

iam_makati alisema,"Ni kama Shakib aliwekwa kwenye picha."

Shabiki mmoja hata hivyo alibainisha kuwa kijana huyo Mganda ana umri wa zaidi ya miaka 30 na akadokeza kuwa dini ya Kiislamu, ambayo ni dini ya Zari na mumewe, inaruhusu mwanamke kuolewa na mwanaume mdogo kiumri.

Zari ambaye alionekana kuvutiwa na maoni ya shabiki huyo alijibu, “Waache wakabwe koo."

Zari Hassan na Shakib walifunga ndoa ya Kiislamu almaarufu Nikkah mwezi uliopita baada ya kuchumbiana kwa takribani mwaka mmoja.

Wawili hao walivishana pete katika hafla ya faraghani ambayo ilihudhuriwa na idadi ndogo ya watu wakiwemo wanafamilia na marafiki.

Katika picha na video hafla hiyo iliyofanyika chumbani ambazo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, wapenzi hao walionekana wamevalia Kiislamu kabisa huku wote wakiwa wameketi kwenye mkeka uliotandikwa sakafuni.

Shakib alionekana akiinama kwa goti moja na kumvisha Zari pete ya ndoa kwa furaha kabla ya wawili hao kupigana mabusu huku watu wachache waliohudhuria hafla hiyo wakiwasherehekea kwa makofi.

Kwa sasa Zari ana umri wa miaka 42 ilhali mume wake Shakib alifikisha miaka 31 mwezi Disemba mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live