Mtaalam wa masuala ya mahusiano, Sheikh Abdulrazack, amesema, kitendo cha Kajala kurudina na Harmonize kwa upande wake hakiafiki kutokana na kosa alilolifanya.
Abdulrazack ameyasema hayo jana alipokuwa akifanya mahojiano na Global TV Online ambapo alisema, Kajala alihitaji mud asana kurudiana na Harmonize.
“Unajua ule ni kama unyanyasaji kwa mtoto, lile kosa ni kubwa, sasa unadhani mtoto sasa hivi atakuwa kwenye hali gani anaweza kufurahia?” alihoji Abdulrazack.
Kajala na Harmonize waliachana kwa kosa la Harmonize kumtongoza Paula ambaye ni binti wa muigizaji huyo. Yapo madai ya kuwa Paula na Harmonize walikuwa wameshafika mbali zaidi kimahusiano.
Hata hivyo, baada ya kipindi fulani kupita, Harmonize aliomba msamaha kwa kutumia nguvu ‘nyingi’ na hatimaye mtoto wa kike akashusha moyo na maisha ya mahusiano kwa sasa yamepamba moto.