Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mume amlipa mwanaume mwingine kulala na mke wake kwa nguvu

DEATHSEX Mume amlipa mwanaume mwingine kulala na mke wake kwa nguvu baada ya harusi yao

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Harusi ni siku ya furaha sana, ni siku watu wawili wapendanao wanaamua kuanza maisha kama wanandoa. Lakini kwa Masika Louise Burene ilikuwa sukari siku moja na shubiri siku ya pili. Ikiwa ni siku moja tu baada ya harusi alipata maumivu, majuto na majonzi ambayo siyo rahisi kusahau.

Masika aliingiliwa bila ridhaa yake yani alibakwa na mwanaume mwingine, ndio hakuwa mume wake. Jambo baya ni kwamba mwanaume huyo alilipwa na mume wake kufanya ukatili huo.

JE NINI KILITOKEA? NDOA ILIVUNJIKA?

Masika kutoka Birere, Goma huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anasema ”Ni ngumu kuweka katika maneno tatizo nililopitia”.

Nilikuwa na mpenzi tuliyejuana kwa miaka mitatu na mahusiano yetu yalienda vizuri wakati wote. Tulikutana chuoni tukapendana sana alinijali na alionekana mwema kwangu na tulipanga kuoana.

Masika akiwa amekaa katika kiti anaeleza huku akilia anasema kuna viashiria aliviona mwanzoni ”red lights” lakini alipuuza, mfano anakumbuka kuna wakati alipoongelea suala la kufunga ndoa, mpenzi wake ni kama alikwepa kuzungumzia suala hilo, ijapokuwa badae alikubali na mipango ya harusi ikaanza.

WALIKUBALIANA KUTOSHIRIKI TENDO LA NDOA HADI HARUSI!

Jambo moja ambalo kwa vijana wa sasa linaweza kuwa sio kawaida, Masika na mpenzi wake walikubaliana kutokushiriki tendo la ndoa hadi pale watakapofunga ndoa takatifu. Anaeleza zaidi kwamba mpenzi wake alimuelewa na hakuwahi kuonyesha dalili zozote za kutaka wafanye tendo hilo.

“Kuna muda nilionyesha kama namuhitaji kwa kumchokoza ili tufanye mapenzi lakini alinikwepa na kusema lazima tusubiri hadi tufunge ndoa”. Masika hakuwaza jambo lolote baya hata baada ya mpenzi wake kukataa jambo hilo aliona ni heshima tu. Kumbe alikuwa anamfuga chatu ambaye alikuja kumtemea sumu kali na kuharibu furaha yake yote.

Vigelegele na Chereko vilisikika, hayawi hayawi sasa yamekuwa. Ilikuwa siku ya harusi, ndugu,jamaa na marafiki walialikwa kusherehekea siku hiyo adhimu. Siku moja baada ya harusi yetu niligundua kuna kitu hakiko sawa alikuwa kama mtu ambaye hajatulia anasema mrembo huyo.

Sasa walikuwa na uhuru kulikuwa hakuna cha kuwazuia kufurahia mapenzi, sasa wamekuwa mwili mmoja. Chako changu na changu chako. Masika anaeleza alianza kumshika mume wake kwa ajili ya tendo hilo ila alimwambia aache kwasababu kwanza ana jambo zuri amemuandalia la kumshangaza ‘surprise’. Masika anasema mume wake alitoka nje na yeye akaenda maliwatoni.

Aliporudi chumbani alipata mshangao. Bado wanandoa hawa walikuwa katika fungate hoteli moja huko mjini Goma. Masika alimkuta mwanaume ambaye hamfahamu akiwa hana nguo yoyote amekaa kitandani na alionekana yupo tayari kufanya ngono. Alianza kumshika msichana huyo, na anaeleza alijitahidi sana kumsukuma lakini mwanaume huyo alimzidi nguvu na kuanza kumbaka.

Alipiga kelele na haraka wahudumu wa hoteli hiyo wakafika. “Ilikuwa ni tukio baya sana kwangu sikuamini kilichotokea, sikujua ni kwanini jambo lile limetokea na kwanini mume wangu niliyemuamini amenitendea vile”

Katika mahojiano na polisi mwanaume huyo aliyetumwa na mume wa Masika anaeleza kwake ilikuwa ni kazi tu. Alilipwa kwa kazi hiyo na anasema mume wa binti huyo alimueleza kwamba anaumwa yani ana tatizo katika maumbile yake ya kiume na asingeweza kufanya chochote na mwanamke huyo.

Sababu ilioje? Kesi ilienda mahakamani lakini mume wa msichana huyo hakujulikana alipo, alikuwa ametoroka na hata wengine walidhani labda atakuwa amejiuwa kutokana na aibu hiyo. Bado haijulikani haswa nini kimempata au yupo wapi. Na pia jumbe mbalimbali kuhusu mipango ya mwanaume huyo mbakaji kupewa kazi hiyo na mume wa Masika zilikutwa kama uthibitisho.

Kaka wa Masika anasema mdogo wake amekuwa katika hali ya majonzi wakati wote. Anaongeza walimpenda sana shemeji yao lakini amewatendea jambo baya, huku akisisitiza ugonjwa ni kitu cha kawaida na kwamba mwanaume huyo angesema tu apate msaada.

Masika anasema anawaasa wasichana wadogo kuwa makini sana kabla ya ndoa.

Lakini matatizo ameumbiwa binadamu pengine hata yeye alikuwa makini sana lakini jambo hilo lilimpata. Mapenzi ni raha na burudani lakini yakiwa na maumivu na usaliti ni zaidi ya siki. Uchungu, uchungu ila wahenga walisema giza lilizidi kunakuwa kumekaribia kukucha. Furaha na amani vinakuwa tena fungu lako.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live