Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mume akikutesa rudi kwenu - Dida

Didaaa Dida Shaibu

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwanini wanawake wengi wanakutana na unyanyasaji kwenye ndoa zao lakini wamekuwa wazito kuachana na wenza wao?

Dida Shaibu amewashauri wanawake wanaoambulia vipigo, matusi na kejeli kwenye ndoa zao badala ya upendo, waache kujiendekeza bali watafute upenyo wa kutoka haraka ili kujinusuru.

"Kwenye mahusiano nipende nikupende, ikifika hatua sijakuelewa siangalii majirani wataongea nini au labda Diamond Platnumz alinipa nini kwenye harusi yangu, sababu nachotaka ni furaha yangu".

"Wewe ndio umeyaishi hayo maisha siyo mtu wa nje, wewe ndio unateseka na kuumia, mume akikupiga na kukutusi hata kama kwenu ni masikini rudi kwenu hujaua wewe, mambo ya kusema utavumilia ndio anaanza kukutukana na kukwambia 'yule hana pa kwenda," amesema Dida.

Kwa upande wako unahisi ni kwanini baadhi ya wanawake wanapitia manyanyaso, vipigo na bado hawataki kutoka kwenye ndoa zao?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live