Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muki afunguka madai ya kuvaliana nguo na Nuh Mziwanda

Muki Na Nuh Muki afunguka madai ya kuvaliana nguo na Nuh Mziwanda

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama utakuwa mtu wa kuzurura sana mitandaoni, hakika utakuwa umekutana na picha ya sweta Fulani hivi ambalo inasemekana, wasanii Muki na Nuh Mziwanda wamevaa kwa nyakati tofauti na mjadala ni kuwa wawili hao wanavaliana.

Muki amefafanua kuhusu mchongo huo kupitia kipindi cha Refresh cha Wasafi TV ambapo amesema, jambo hilo huwenda limetokea kwa sababu, dizaina wao ni mmoja licha ya kukiri kwamba yeye na Nuh ni washkaji.

“Kweli Nuh ni mshkaji wangu lakini hatujafikia kuvaliana na kuposti kwenye mitandao, ninachokiona hapo ni dizaina wetu ambaye mimi huwa ananivalisha kwa ajili ya kuposti mitandaoni.

“Alinivalisha mimi halafu akamvalisha pia nguo hiyo hiyo Nuh. Na kuna nguo pia niliona aliwahi kumpa Ebitoke, nguo nilivaa mimi kisha nikashangaa baadaye kaivaa Ebitoke,” alisema Muki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live