Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji wa Squid game O Yeong-su ashtakiwa kwa unyayasaji wa kingono

Muigizaji Wa Squid Game O Yeong Su Ashtakiwa Kwa Unyayasaji Wa Kingono Muigizaji wa Squid game O Yeong-su ashtakiwa kwa unyayasaji wa kingono

Mon, 28 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Muigizaji wa Squid Game O Yeong-su ameshtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono, maafisa wa mahakama wa Korea Kusini wanasema.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 78 anatuhumiwa kumgusa mwanamke isivyofaa mnamo 2017, maafisa walisema.

Bw O amekanusha madai hayo, vyombo vya habari vimeripoti.

Alikuwa mwigizaji wa kwanza wa Korea Kusini kushinda tuzo ya Golden Globe ya mwigizaji msaidizi bora katika mfululizo baada ya kuigiza katika tamthilia ya kusisimua kwenye Netflix mapema mwaka huu.

Mshukiwa huyo aliwasilisha malalamishi kwa polisi kwa mara ya kwanza dhidi ya Bw O mnamo Desemba mwaka jana, kulingana na shirika la habari la Yonhap.

Lakini kesi hiyo ilifungwa Aprili bila kufunguliwa mashtaka dhidi ya Bw O.

Upande wa mashtaka sasa umefungua upya uchunguzi "kwa ombi la mwathiriwa", shirika hilo linaripoti.

Bw O sasa amefunguliwa mashtaka bila kuzuiliwa, inaongeza.

Kufuatia shtaka hilo, wizara ya utamaduni ya Seoul iliamua kuacha kupeperusha matangazo ya serikali iliyomshirikisha Bw O, kulingana na ripoti za eneo hilo zilizotajwa na shirika la habari la AFP.

Tamthilia ya Squid Game- mfululizo maarufu zaidi wa Netflix wa wakati wote - ni mfululizo wa kusisimua ambao unasimulia hadithi ya watu walio na madeni wakishindania zawadi kubwa ya pesa katika mfululizo wa michezo hatari ya watoto.

Bw O anacheza mshiriki mzee zaidi katika shindano la kuishi.

Chanzo: Bbc