Muigizaji wa Marekani Jeremy Renner amewashukuru mashabiki wake kwa kumpa pole baada ya kujeruhiwa vibaya na jembe la theluji.
Aliweka picha ya uso wake wenye makovu kwenye Instagram, Renner alisema "hayuko vizuri kwa sasa hawezi hata kuandika".
Nyota huyo wa Avengers alipelekwa hospitalini Jumapili baada ya ajali hiyo nje ya nyumba yake huko Reno, Nevada.
Renner aliangukiwa na jembe lake la theluji, ambalo lina uzani wa karibu 14,330lb (6,500kg) - mara tatu ya uzito wa gari - polisi wa eneo hilo alisema.
Alipata majeraha kifuani na majeraha ya mifupa, msemaji wake alisema Jumatatu.
Wakati huo alikuwa katika hali nzuri lakini katika uangalizi maalum wa wauguzi.
Katika mtandao wa Instagram akiwa kwenye kitanda cha hospitalini Jumanne jioni, Renner mwenye umri wa miaka 51, aliandika: "Asanteni nyote kwa maneno yenu ya fadhila. Siko vizuri sasa nashindwa kuandika. Lakini ninatuma salamu za upendo kwenu wote.