Aliekuwa mke wa staa wa filamu baada ya kupewa talaka amemtaka nyota huyo kutoa kiasi cha pesa cha $248k (Sh.Milioni 594+) kama pesa ya matunzo ya watoto.
Staa huyo wa filamu hajakubaliana na suala hilo huku akisema kuwa mwanamke huyo anachotaka kukifanya ni kitendo cha wizi na sio sawa.
Christine Baumgarther aliwasilisha karatasi mpya za kisheria ambapo ameiomba mahakama iamuru KC kutoa kiasi hicho cha pesa kila Mwezi kama pesa ya matumizi ya watoto wao watatu.
Mbali na hivyo amedai kuwa kiasi hicho cha pesa kitakuwa njee ya ada ya shule huduma za kiafya na gharama zinazohusiana na michezo hivyo kuna pesa nyingine anatakiwa kuwa anatoa.