Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji Mkongwe wa Nigeria afariki Dunia

Veteran Nollywood Actor Pa Zulu Adigwe Reportedly Passes On Muigizaji mkongwe wa filamu za kinigeria, Zulu Adigwe amefariki dunia

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji mkongwe wa filamu za kinigeria, Zulu Adigwe amefariki dunia.

Kifo cha muigizaji huyo kilitokea jana Jumanne jioni na kilitangazwa kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa mtayarishaji wa Filamu, Stanley Nwoko.

“Nasikitika kutangaza kifo cha muigizaji mkongwe, marehemu Bw Zulu Adigwe"

"Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika. Pumzika kwa amani,” aliandika Stanley Nwoko.

Wakati wa uhai wake, Adigwe alikuwa maarufu katika filamu: “Living in Bondage”, “Breaking Free” na nyingine nyingi.

Nollywood imepoteza waigizaji wake saba mwaka huu 2024, ambao ni Sisi Quadri, Mr Ibu, Amaechi Muonagor, Andy Best, Jumoke Aderounmu na Junior Pope.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live