Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji Miller agoma kufanya kazi na muongozaji Deadpool

Batch WhatsApp Image 2022 10 12 At 11.10.36 AM.jpeg Muigizaji Miller agoma kufanya kazi na muongozaji Deadpool

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: Globalpublishers

Muigizaji wa sinema Todd Joseph Miller ambaye hucheza kama Weasel amesema hawezi kufanya kazi na muongozaji filamu ya Deadpool Ryan Reynolds sababu alikuwa akimletea jeuri kwenye seti ya sinema hiyo, alimwambia maneno yalimfanya Todd kujihisi vibaya na kutotaka kufanya kazi na Reynolds katika filamu nyingine yoyote itakayo jitokeza.

Miller amesema kuwa anampenda sana Ryan Reynolds lakini anahisi kuwa amebadilika sana toka awe maarufu baada ya sinema ya Deadpool ya kwanza kiasi cha kwamba amekuwa akimtania kwa kumuita Weasel hata kama hawapo kwenye maigizo, Reynolds alimwambia maneno haya Miller:

"Unajua ni kitu gani kuhusu wewe ni bora Weasel? Wewe sio bingwa lakini unafanya ufafanuzi wa kutosha ilimradi uchekeshe halafu tunaacha kipande chako na kurudi kwenye sinema halisi.”

Kwa maneno haya Reynolds alikuwa akimuonesha muigizaji Miller kuwa hana sehemu kubwa ya kucheza katika sinema hiyo na kuwa hana umuhimu kama alivyokuwa yeye, maneno haya yalimfanya Miller ajisikie vibaya kwa kuwa hakutegemea kushushwa hadhi na mtu aliyemchukulia kama rafiki yake.

Miller amedhihirisha haikuwa ni uzoefu mzuri kataika kazi na hata wafanyakazi wenzao kwenye sinema hawakujua jinsi ya kujibu kipindi tukio hilo likitokea, ingawa Miller hajaitwa kufanya kazi ya kuigiza katika filamu mpya ya Deadpool 3 ambayo itatoka mwaka 2024, lakini yeye hana hamu ya kufanya tena kazi na Reynolds hata kama wakimpa hela mara mbili ya walivokuwa wakimlipa hapo mwanzo.

Mwakilishi wa Miller hakuwa na neno la kusema kwa maoni aliyotoa Miller sababu anadaiwa kuwa na utovu wa nidhamu miaka ya hivi karibuni aidha mwaka 2017, Miller alishtakiwa na binti aliyekuwa naye kimapenzi kipindi akiwa anasoma chuo kwa unyanyasaji wa kijinsia ingawa Miller alikata mashtaka hayo kuwa siyo ya kweli.

Katika mwaka wa 2018, mwigizaji mwenza wa Miller kwenye sinema ya Silicone Valley Alice Wetterlund alikuwa na maneno haya ya kusema juu ya muigizaji miller katika mtandao wa twitter:

"Nashukuru, natumai sitokuhalibia lakini, TJ Miller alikuwa ni mnyanyasaji na mtoto mtupu mwenye tabia mbovu na watu wote waliokuwa na nguvu juu ya hilo (karibia wanaume wote) kwenye seti, na ikiwemo pia waigizaji wa kiume wote, walimruhusu na kushirikiana naye katika ukosefu wa taaluma kama hiyo, wote waende zao huko.”

Alice Wetterlund alisisitiza katika maelezo yake kuwa hata wanaume aliyokuwa akifanya nao kazi walilifaham hilo lakini hakuna aliyefanya kitu kwa maana kwamba ni kama vile walikuwa wakishirikiana naye.

Chanzo: Globalpublishers