Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muigizaji Marekani apata mtoto wa pili akiwa na miaka 51

Gettyimages 537759492 Muigizaji Maarufu wa Hollywood Cameron Diaz (51) na Mumewe Mwanamuziki Benji Madden

Sun, 24 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji Maarufu wa Hollywood Cameron Diaz (51) na Mumewe Mwanamuziki Benji Madden (45) wametangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili.

Kupitia mtandao wa Instagram wawili hao waliandika “ tunayo baraka na furaha kutangaza kuzaliwa kwa mtoto wetu wa kiume Cardinal Madden”

“Tuna furaha kubwa, ila kwa usalama na faragha ya mtoto hatutoposti picha zozote, ila ni mzuri sana”.

“Salamu nyingi za upendo kutoka kwenye familia yetu kwenda kwenu, na kila la kheri”.

Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2015 na walijaliwa kupata mtoto wao wa kwanza ambaye ni binti aitwaye Raddix mnamo Disemba mwaka 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live